About Me

header ads

WAZIRI WA NISHATI JANUARY MAKAMBA MGENI RASMI KONGAMANO LA.NISHATI SAFI

 

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv

KUFUATIA mjadala wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia na azma iliyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumnusuru mama na kuokoa muda wa kwenda kusenya kuni za kupikia sehemu mbalimbali Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TABWA), imeandaa Kongamano kubwa la Nishati Safi ya Kupikia lililopangwa kufanyika kati ya Juni 22 hadi 24 mwaka huu kwenye Ukumbi wa SuperDome Masaki Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa TBWA Noreen Mawalla amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Juni 12 2023.

Amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kutoa elimu, kupanga mikakati ya utekelezaji na kujenga mtandao wa biashara kwa ujumla .

Amesema kuwa kongamano hilo limewalenga zaidi wanawake, vjana, wauza mkaa, watengenezaji na wauzaji wa majiko ya nishati safi, wamiliki wa migahawa, shule, hoteli, vyuo,wataalamu wa afya na mazingira pamoja na wadau wengine wote tunawakaribisha sana .

"Tunawakaribisha wadau wote ili waweze kuja kwa ajili ya kupata elimi na kujenga mtandao wa kibiashara kupitia nishati safi ya kupikia"amesema Mkurugenzi huyo wa TABWA Mawalla.

Post a Comment

0 Comments