NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MBUNGE wa Jimbo la Mbagala jijini Dar es Salaam, Mhe. Abdallah Chaurembo amewaambia wapiga kura wake wa Mbagala Kiburugwa kujiandaa na zoezi la urasimishaji ardhi/majengo linalotarajiwa kuanza hivi karibuni kwenye eneo hilo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa Serikali ya mtaa wa Kiburugwa kwenye viwanja vya Kwa-Njau, Juni 4, 2023, Mhe. Chaurembo alisema urasimishaji wa ardhi/majengo ni kutambua miliki za wananchi kwenye maeneo yaliyoendelezwa bila kupimwa kisheria.
“Wengi wenu mnamiliki ardhi au nyumba kwa kutumia makaratasi mliyoandikishiana ambayo hayatambuliki kisheria na baadhi yenu mna leseni za makazi ambazo zilikuwa za kipindi cha muda fulani na nyingi zimekwisha muda wake na matokeo ya urasimishaji ni kutoa hatimiliki inayotambulika kisheria.” Alifafanua.
Alisema zoezi hilo ni shirikishi na kwamba wananchi wakiafiki, wataletwa wataalamu wa upimaji ardhi na kutoa elimu ya jinsi zoezi hilo litakavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na gharama ambazo mwananchi anapaswa kuchangia ili ardhi/jengo lake liweze kupimwa na kupatiwa hati miliki ya serikali.
Alisema urasimishaji mbali na kuipa thamani ardhi/nyumba lakini pia utasaidia kuboresha makazi hususan kwa kuweka miundombinu ya msingi ili kurahisisha usafiri, kupunguza madhara yatokanayo na majanga mbalimbali kama vile mafuriko na moto.
Zoezi la urasimishaji lilizinduliwa mwaka 2013 na aliyekuwa waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Mhe. William Lukuvi na limefanyika maeneo mbalimbali ya nchi na lengo lilikuwa ifikapo mwaka huu wa 2023 liwe limekamilika.
Awali Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kiburugwa Bw. Abdallah Mpili pamoja na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu mtaa huo ikiwemo masuala ya ulinzi jamii, usafi wa mazingira, ujenzi wa ofisi ya Srrikali ya mtaa, aliwahakikishia wananchi kuwa zoezi hilo litafanyika kwa uwazi na kwa kushirikisha wananchi.
“Wapima ardhi watakapokuja hapa tutajadiliana nao na kukubaliana jinsi zoezi litakavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na gharama ambazo kila mwananchi (mwenye ardhi.nyumba) atapaswa kuchangia."
Alisema tayari mitaa jirani na mtaa huo wameshafanya zoezi hilo.
MBUNGE wa Jimbo la Mbagala jijini Dar es Salaam, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na wapiga kura wake wa Mtaa wa Kiburugwa Juni 4, 2023. (PICHA ZOTE NA YASIN KANYAMA)
MBUNGE wa Jimbo la Mbagala jijini Dar es Salaam, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na wapiga kura wake wa Mtaa wa Kiburugwa Juni 4, 2023
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kiburugwa waliohudhuria kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kiburugwa Bw. Abdallah Mpili (aliyesimama) akiwahutubia wananchi wa mtaa wake Juni 4, 2023.

0 Comments