Na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA)imeweka wazi kwamba itaendelea kuwawekea mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa usambazaji, vitendanishi na vifaa tiba kwa lengo kuwawezesha kufanyabiashara hiyo na hatimaye kuinua uchumi kwa ujumla.
Akizungumza leo Juni 27, 2023 jijini Dar es Salaam kwenye mkutano uliohusosha wasambazaji na wauzaji wa vifaa tiba, vitendanishi pamoja na dawa Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki Adonis Bitegeko amesisitiza TMDA itahakikisha inaendana na dhamira ya Awamu ya Sita katika kuwainua wafanyabiashara nchini.
Amefafanua kwamba TMDA wanatekeleza kwa vitendo dhana ya kuwainua wafanyabiasha hao , hivyo wamekutana na wadau hao kwa ajili ya kujengeana uwezo na kubadilisha mawazo huku akisema kwa kutambua umuhimu wa wadau hao ndio maana hakuna msambazaji wa vifaa tiba waliyemfungia.
" TMDA tumejikita katika kutoa elimu ikiwemo kwa watoa huduma na kwetu sisi ni huduma mbele na kuwashawishi wafanyabihashara wafanye kazi kwa weledi, "amesema na kuongeza kwamba anawashauri wananchi kuamini huduma zinazotolewa kwani Mamlaka hiyo inaheshimika Afrika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafamasia Tanzania Churchill Katazwa amesema wao moja ya jukumu lao ni uagizaji wa dawa , vitendanishi na vifaa tiba kwa ujumla wake na kisha wanavisambaza kwa wanunuzi wa kati, wanaitwa wanunuzi wa jumla jumla ambao wako Dar es Salaam na wa mikoani mingine.
"Huu mkutano sisi unatusaidia kwasababu TMDA wanatupanua ufahamu wa kujua kitu gani unatakiwa kufanya wakati unataka kuingiza vifaa tiba, vitendanishi kwasababu sio wote wanasoma sheria zao au muongozo ambayo imeiweka kwenye mitandao ya jamii
"Sasa kwa kuwa watu wako na shughuli nyingi , wengine hawana huo uelewa , kwa hiyo unakuta mtu anakwenda nje au anaagiza kitu bila utaratibu akifika Uwanja wa Ndege au bandarini anakwama kwasababu hawa TMDA watahitaji kukipitia kukiangalia na kabla ya hapo inabidi uombe kibali kwao.
"Kwa hiyo yeye akileta pale hakijasaliwa , hivyo kinakwama na inakuwa hasara kwake , na matokeo yake ni manung'uniko , hivyo ili hayo kuyaondoa ndio maana wanatuita na kukaa nao , kujadiliana nao kuona ni njia gani salama na nzuri sisi wafanyabiashara nao twende vipi ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wetu kwa vifaaa tunavyoagiza, " amesema Katazwa.
Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko akifungua kikao kazi cha wadau wa mamlaka hiyo kilichofanyikakwenye ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko akisisitiza jambo baada ya kufungua kikao kazi cha wadau wa mamlaka hiyo kilichofanyikakwenye ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es Salaam. kushoto Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba na Vitendanishi TMDA,Rehema Mariki na kulia Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA ,Roberta Feruzi.
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV .
Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba na Vitendanishi TMDA , Rehema Mariki akiwasilisha mada kwa wadau wa TMDA leo katika kikao hicho.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA,Roberta Feruzi (kushoto) akitoa maelezo namna walivyo jipanga kuwahudumia wadau hao wakati wa kikao kazi hicho.
Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko akuwa katika picha ya pamoja na watumishi wa (TMDA)
Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko akiwa katika picha ya pamoja na wadau.
0 Comments