About Me

header ads

CHONGOLO AWATAKA WANANCHI WA MAENEO YANAYOPAKANA NA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO KUHESHIMU TARATIBU ZA KISHERIA ZA NCHI

 

*Agusia umuhimu wa miradi yenye tija kwa wananchi kutekelezwa haraka

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Chamwino

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema umefika wakati wa kuwaza zaidi katika kuongeza uzalishaji wa Wine huku akishauri mchuzi wa Zabibu iangaliwe namna ya kuwezesha wafanyabiashara wadogo kuwa na viwanda vya kuchakata na kutengeza Wine zenye brand zao.

Chongo ameyasema hayo leo Juni 18,2023 alipotembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Jenga Kesho Bora uliopo eneo la Chinangali wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Akiwa katika mradi huo licha ya kutoa maelekezo kwa wizara ya Kilimo kukaa na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kufanikisha miradi yenye tija kwa wananchi, amezungumzia pia kilimo cha Zabibu ambacho kinalimwa kwa wingi katika wilaya ya Chamwino na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla.

“Niipongeze Wizara ya Kilimo na Chama chenu cha Ushirika kwa jitihada ambazo mnaendelea nazo, lakini hapa Chamwino ndiko kwenye kitovu cha kilimo cha Zabibu ambayo inatumika kutengeneza Wine ikiwemo ya Dodoma Wine na aina nyingine kama tano au sita hivi.

“Nimesikia hapa mmezungumzia mipango na mambo mengine , niseme tu ni lazima tuache kufikiria ununuzi wa Zabibu yetu kutoka nje ya hapa , lazima mtazamo uwepo kwa uzalishaji wa Zabibu.Hata hivyo tujiulize sisi tunachangia asilimia ngapi ya hiyo Wine inayonyweka hapa nchini inayotokana na uzalishaji wa ndani , nadhani ni ndogo sana, kwa hiyo ni vema tukaweka nguvu ya kuimarisha soko la ndani,”amesema Chongolo.

Ameongeza kuwa upo uwezo wa kufanya makubwa zaidi huku akifafanua Wizara imeanza mpango wa kujenga kiwanga pamoja na matenki ya kuhifadhia mvinyo.

“Niseme tu twende mbali zaidi huo mchuzi wa zabibu tuangalie namna ya kuwezesha wafanyabiashara wadogo kuwa na viwanda vya kuchakata huo mchuzi kwenda kwenye Wine na kila mmoja kwa brand yake  na ikitoka hapa  kwa wingi kila mmoja atatafuta masoko.Niwahakikishie nchi yetu itapata soko la uhakika.”

Katika hatua nyingine Chongolo amezungumzia mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji wa Jenga Kesho Bora uliopo Chinangali ambapo ametoa maelekezo kwa Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha kukaa na kisha kuja na majibu ya namna ya kuufanikisha mradi huo kukamilika kwa wakati.

“Nimisikia kuna changamoto hapa kidogo, nendeni mkae Wizara ya kilimo pamoja na Wizara ya Fedha, dhamira ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwenye hii miradi ni kuona tija inapatikana haraka.Yule mkandarasi pale Mkombozi tunaona ameweka nguvu anatafuta matokeo kwa haraka.

“Naona Wizara ya Kilimo mnavyokimbizana kupambana lakini sisi kazi yetu ni kutatua na kukwamjua mahali kunakokwama, nimezungumza asubuhi hii na Waziri wa Fedha nikamuuliza nini shida akanambia nisiwe na wasiwasi ataliweka sawa.

“Kwa hiyo nendeni mkakae na mje na majibu ndani ya kipindi kifupi ni namna gani mtakwenda spidi ya utekelezaji wa miradi hii ambayo inadhaamira ya kujenga uhakika wa kilimo cha umwagiliaji kwa wananchi ili malengo ya Rais na Serikali anayoingoza yafikiwe kwa muda unaotakiwa,”amesema.

Chongolo amesema hakutakuwa na maana kuwa na majina ya miradi mizuri yenye dhamira njema halafu isilete matokeo kwa wakati , hivyo lazima wakae haraka huku akieleza kama kuna changamoto ni vema ikaelezwa mapema ili waone namna ya kuitatua.





Post a Comment

0 Comments