About Me

header ads

MVOMERO YAIPONGEZA SUA KWA TAFITI BORA ZA KUINUA KILIMO NCHINI

 

Na: Amina Hezron, Morogoro

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Mhe. Judith Nguli amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kufanya Tafiti za kisayansi zenye kusaidia kuinua tija katika kilimo na ufugaji nchini.

juu ya ambayo itakuja na majibu sahihi na kwenda kuijenga jamii kwenye maswala hayo.

Mhe. Nguli ametoa pongezi hizo wakati alipokuwa akifungua warsha iliyokutanisha wadau wa kilimo kwaajili ya kutoa mrejesho wa utafitiuliohusu Utayarishaji Shirikishi wa Huduma za Hali ya Hewa ili Kuboresha Uhakika wa Chakula, Lishe na Afya nchini Tanzania.

Amesema swala hilo matokeo hayo yamekuja wakati muafaka kwakuwa wilaya ya Mvomero ni moja kati ya maeneo yanayopitia changamoto ya Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Hali ya Hewa kwa ujumla hivyo yatasaidia katika wananchi kufahamu vyema na kushiriki kikamilifu katika matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kilimo.

“Ni ukweli usiopingika sisi Wilaya ya Mvomero ni waathirika wakubwa katika maswala mazima ya mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa na yametuathiri sana ukipita au kutembea katika maeneo yetu, kata zetu utaona namna gani swala hili lilivyotuathiri lakini matokeo haya yamekuja kwetu kwa muda muafaka” amesema Mhe. Nguli.

Aidha ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kujipanga zaidi ili kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa wanazotoa zinawafikia vizuri na kwa usahihi Wananchi wa hali ya chini ili waweze kupanda kulingana na wakati kulingana na msimu husika.

“Pamoja kwamba wanatoa taarifa tunaziona lakini wajaribu tena kujipanga zaidi na zaidi ili kuona taarifa hizo zinamkutaje Mwananchi lakini pia wale tunaowapa taarifa katika ngazi za Halmashauri pia jaribuni kufatilia kujua kama zinawafikia kwa wakati sahihi, kwasababu inawezekana zinakuja

lakini zisifike kwa wakati au ndio zikaishia hukohuko kwenye Email za kwenye Computer zao”, aliongezea Mhe.Nguli.

Akizungumza juu ya manufaa waliyopata wananchi kutokana na utekelezwaji wa mradi huo katika wilaya ya Mvomero na Mlimba Kaimu Mratibu wa Mradi kutoka (SUA) Dkt. Sylvester Haule amesema kuwa kwa sasa Wananchi hao wanafikiwa na taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazolenga eneo dogo na si eneo kubwa kama ilivyokuwa hapo awali ambazo kuaminika kwake kunakuwa kukubwa.

“Kwahiyo mkulima anaweza akajua kuwa msimu huu labda mvua zitakuwa ni kidogo kwa maana hiyo basi ataangalia mazao ambayo yanaweza kustahamili hizo mvua kidogo au labda mvua zitakuwa ni nyingi zitanyesha kwa muda mfupi basi tuyahifadhi maji hayo au tupande mazao ya muda mrefu pia sio ya muda mfupi” alifafanua Dkt. Haule.

Aliongeza “Na kwa baadhi ya mawasilisho ambayo yamewasilishwa kuna hatua mbalimbali zimefanywa kwa mfano katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwenye vijiji kama Melela tayari tumeshaona wameshaanza kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji”.

Amesema wakulima wananufaika kutokana na uelewa ambao tayari wameshakuwa nao kuhusu matumizi ya taarifa na huduma za hali ya hewa pia wamehamasika katika kuzitafuta na kuzifwata taarifa za hali ya hewa na inaleta urahisi kwa wazalishaji na wachakataji.

Mradi huu wa miaka miwili umekuwa ukitekelezwa kuanzia mwezi Aprili 2021, na kumalizika 2023 kwa ushirikiano baina ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Taasisi ya Michelsen (CMI) ya nchini Norway, Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Tabianchi na Mazingira (CICERO) ya Norway, kituo cha Utafiti cha Norway (NORCE) Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Taasisi nyinginezo zilizoko Norway.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli ,Wadau wa kilimo na Waratibu wa Mradi wa Utayarishaji Shirikishi wa Huduma za Hali ya Hewa ili Kuboresha Uhakika wa Chakula, Lishe na Afya nchini Tanzania


Wadau wa Kilimo wakijadiliana namna sahihi ya kumsaidia mkulima kupata taarifa sahihi na kwa wakati ya utabiri wa hali ya hewa.

Post a Comment

0 Comments