Na: Amina Hezron, Morogoro.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya Tani elfu mbili za Nyamapori inayowindwa kiharamu kupitia ujangili kwenye maeneo yaliyohifadhiwa yenye thamaniya dollar za Kimarekani milioni 50 hukamatwa kila mwaka nchini na hivyo kukwamisha juhudi za uhifadhi wa Wanyama hao.
Hayo yamebainishwa na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Dkt. Charles Mgeni kupitia wasilisho la utafiti wa awali wa Mradi wa Utafiti wa Biashaara, Maendeleo na Mazingira (TRADE Hub) unaotekelezwa na Chuo hicho, uliofanya Tathimini ya awali ya urasimishaji
wa biashara ya Nyamapori kama inaweza kupunguza ujangili nchini.
Amesema tafiti zinaonesha kuwa biashara hiyo ya Nyamapori haiishii ndani ya Tanzania na Afrika pekee bali huvuka hata mipaka ya Afrika na hii ni baada ya kuripotiwa kukamatwa kwa nyama hiyo kwenye mabegi nchini Ufaransa kwenye uwanja wa ndege ikionesha kuwa ainatoka Afrika.
“Katika swala hili Waataaluma wamegawanyika katika makundi mawili katika mawazo ya kitafiti ya namna ya kumaliza tatizo la ujangili ambapo kundi la kwanza linapendekeza kuweka sheria kali za kuzuia uuzwaji wa Nyamapori na bidhaa zake huku kundi la pili wakipendekeza urasimishwaji
wa biashara hiyo ili kuzuia ujangili”, alieleza Dkt. Mgeni.
Akifafanua Mawazo ya kundi la kwanza amesema kuwa linaona uzuiaji wa biashara hiyo kwa kuweka sheria ngumu na kali utasaidia kupunguza ujangili na hasa ikizingatiwa kuwa nyama hiyo isiyopimwa na kuangaliwa vizuri inaweza kusababisha athari za kiafaya kwa watumiaji kutokana na
magonjwa mengi ya Wanyama huambukiza binadamu kama vile ebola,
HIV,Uviko na mengine.
Aidha amesema kundi la pili la Wanazuoni linalopendekeza kurasimisha lionana biashara hiyo itakuwa tiba ya tatizo la ujangili kwakuwa Wananchi hawatakuwa na sababu ya kwenda kufanya ujangili kwani Nyamapori itapatikana kwenye mabucha kihalali kupitia uvunaji endelevu na hivyo
jamii itaona faida ya kutunza maliasili hiyo kwa kupata kipato na chakula.
Mtafiti huyo amesema pamoja na kuwa na makundi hayo mawili lakini Wanazuoni wengi wanapendekeza njia ya pili ya urasimishaji wa biashara ya Nyamapori inaweza kuwa muafaka kwani jamii itajiona ina wajibu wa kutunza maliasili kwakuwa wanafaidi matunda ya Wanyama hao kwa
kuwapa kipato, Ajira na mboga katika maeneo ambayo yanazunguka hifadhi.
Amesema mapendekezo hayo ya wanazuoni wengi pengine ndiyo yalimsukuma Rais wa awamu ya tano Marehemu John Pombe Magufuli kutangaza urasimishaji huo na uanzishwaji wa mabucha ya Nyamapori na kuitaka wizara na taasisi za usimamzizi kuweka miongozo ya ufanyikaji wa
biashara hiyo hapa nchini.
Dkt. Mgeni amesema kupitia mradi huo wa TRADE Hub wameona wafanye tathimini ya kina kuangalia namna biashara hivyo inavyofanyika katika maeneo mbalimbali nchini lakini pia kuangalia taratibu,kanuni na mifumo ya uendeshaji wa biashara hiyo ilivyowekwa ili ifanyike vizuri kwa kukutana na wadau wote katika ngazi na mamlaka mbalimbali.
Matokeo yamebainisha kuwa ujangili kwenye maeneo ya hifadhi umepungua kwa zaidi ya asilimia 58 huku zaidi ya asilimia 83 ya Wananchi wakionekana kupenda nyamapori kuliko nyama zingine kama vile mbuzi na ngombe na hivyo kuonesha uhitaji ni mkubwa wa nyamapori katika jamii.
Amesema asilimia 54 walionesha kuwa utaratibu wa kupata kibali cha kufungu mabucha walisema upo vizuri huku lakini mifumo ya upatiakanaji wa nyamapori kwaajili ya kuuza kwenye mabucha hayo ndio umekuwa mgumu na hivyo kusababisha zaid ya asilimia 7o ya waliofungua bucha hizo
kukosa nyama kabisa mwaka mzima.
Amesema kupitia utafiti huo wamebaini kuwa urasimishaji wa Nyamapori unaweza kupunguza ujangili nchini kuwa na mchango chanya katika uhifadhi nchini endapo utaratibu,kanuni na miongozo ya usimamiaji biashara hiyo itawekwa vizuri na kutafuatwa.
Aidha kupitia utafiti huo wametoa angalizo na usimamizi mzuri kwakuwa kurasimisha kunaweza pia kuongeza ujangili kwakuwa majangili watawinda na kwenda kuwauzia nyama wenye mabucha ambao wanaweza kuwa sio waaminifu na hivyo kuwapatia majangili soko la uhakika la nyama
zao wanzowinda.
Hivyo utafiti huo umezitaka mamlaka za usimamizi kukaa chini na wadau wa nyamapori na kuweka taratibu nzuri ambazo zitawezesha ufanyikaji wa biashara hiyo kwa haki ili iweze kuwa endelevu na kutimiza kusudi la uanzishwaji wake.
Kwa upande wake mmoja wa wamilikiwa bucha Nyamapori jijini Arusha bwana Francis Kisela amesema changamoto kubwa waliyonayo ni upatikanaji wa nyama hiyo kutokana na kutegemea kuipata kupitia
wanyama waharibifu na wale ambao wamepigwa na mamlaka kutokana na kuleta athari kwa watu hali ambayo haikidhi mahitaji kutokana na wenye mabucha kuwa wengi kwa sasa.
“Pamoja na kupatikana wanyama pia tunaiomba Serikali na Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori (TAWA) kuona uwezekano wa kubadilisha sheria na miongozo yake kuweza kuruhusu sisi kusambaza nyama kwenye mahoteli,migahawa na Baa ambazo zinahitaji kuuza nyamapori kwa wateja wake maana kwa sasa sheria inatuzuia tunauza kwa matumii ya familia tuu nasio kibiashara”, aliomba bwana Kisera.
Bwana Kisera ameomba pia mamlaka kuona uwezekano wa kuwasaidia kupata nyama kutoka kwa Uwindaji wa kitalii ambao huchukua nyara na kuacha nyama ili waweze kuitumia kuuzia jamii na wao kufanya biashara kwa makubaliano fulani kati ya pande hizo mbili kutokana na sheria yao pia
kutowaruhusu wawindaji hao wa kitalii kuwauzia nyama wenye mabucha.
Nae mzee Aliphas Nassary ambaye nae alihamasika kufungua bucha ya kuuza nyamapori amesema kwake imekuwa hasara kubwa kwani pamojana kutumia gharama kubwa kutengeneza bucha kufikia viwango
vinavyotakiwa na kupata leseni na vibali vyote lakini hajawahi kupata
nyama ya kuuza kwenye bucha yake.
Mradi wa Utafiti wa Biashara,Maendelo na Mazingira (TRADE Hub)ni mradi wa miaka mitano unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana Taasisi zingine zaidi ya 50 duniani na kutoka katika nchi 15 za Afrika, Asia, Uingereza na Brazil na kufadhiliwa
na Mfuko wa Utafiti wa Changamoto za Kidunia wa Serikali ya Uingereza
(UKGCRF) na Mfuko wa Pamoja wa Utafiti na Ubunifu (UKRI).
0 Comments