Na Shushu Joel, Kisarawe.
MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Bi Subira Mgalu amewatembelea kina Mama waliokuwa katika hodi ya wazazi katika hospital ya wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Mhe. Subira Mgalu Mbunge wa Mkoa wa Pwani akimbeba mtoto kwa mama aliyejifungua mapacha katika hospital ya Kisarawe ( NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na wagonjwa mbalimbali waliokuwa wamelazwa mara baada ya kujifungua na wale ambao walikuwa wakisubilia muda wao ufike ili wajifungie ,Mgalu alisema kuwa amefanya hivyo ili kuwapatia Mkono wa Eid wale wote waliokuwepo katika hospital hiyo ili nao wajisikie vizuri pale wanapopatiwa faraja na viongozi wao.
Alisema kuwa kipindi hiki cha uongozi wa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan mambo yamebadilika sana kwenye sejta ya Afya kwani huduma zimekuwa safi na za kuvutia sana kwa jamii.
" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akipambana kuhakikisha vifo vya kina Mama vinakuwa ziro na kwa hali niliyoikuta hapa kisarawe inawezekana" Alisema Mhe. Mgalu.
Aidha Mhe Mbunge wa Mkoa huo wa Pwani Bi Mgalu amewapatia mkono wa Eid wagonjwa mbalimbali waliokuwa kwenye hodi hizo kwa kuwapatia sabuni, Pempasi za watoto na nauli za kurudia majumbani pindi watakqporuhusiwa kurudi majumbani kwao na pia kuwakumbusha malezi bora kwa watoto wao waliowapata.
Kwa upande wake muuguzi wa zamu katika hodi hiyo Zepfania William amempongeza Mhe. Subira Mgalu kwa moyo wake wa kujitoa kwa jamii kwani amewagawia mkono wa Eid kina Mama wengi walikuwepo hospital.
Pia amewataka viongozi kuiga mfano wa subira Mgalu mbunge kwani mtu unapotoa unapata mibaraka mingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Naye mmoja wa mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Mama wawili amemsifu Mbunge wa Mkoa Bi, Subira Mgalu kwa mkono wa Eid na hata kuwajulia hali kina Mama waliojifungua katika hospital ya Kisarawe.
Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za Afya kwa kina Mama kwani wanajifungua mahali salama sana.
0 Comments