Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva akiambatana na kamati ya Usalama, Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Ludewa, na Mbunge wa Jimbo la Ludewa wameupokea Mwenge wa Uhuru ambao umekimbizwa, kutembelea, kukagua na kupitia miradi nane (8) ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya Tsh. 2,242,304,474.57
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe Mwanziva amekabidhiwa Mwenge wa uhuru na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Ndugu. Judica Omary akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe 25/04/2023 ukitokea mkoani Ruvuma na kuifanya wilaya ya Ludewa kuwa wilaya ya kwanza kukimbiza Mwenge mkoani Njombe.
Aidha, Mbio za Mwenge zimeanzia kijiji cha Ngelenge Kata ya Ruhuhu na kumalizikia kata Mlangali wakati Miradi yote ikiwa imeridhiwa na mkimbiza Mwenge wa Uhuru ambapo umezungumza jumla ya Kilometa 173 na kumulika, kuangaza, kuleta tumaini, faraja na furaha kubwa Wilayani Ludewa.
Katika hatua nyingine Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa Cde Abdalla Shaibu Kaimu ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Ludewa inayoongozwa na DC Mwanziva kwa usimamizi mzuri wa miradi na maandalizi mazuri ya tukio la mbio za Mwenge zenye hamasa na shamrashamra.
0 Comments