Wateja wa Airtel Timiza akiba kujishindia Bajaji, Pikipiki, Luninga pamoja Pesa Taslim kwa kujiwekea akiba
Dar es Salaam, Jumanne tarehe 28 Machi 2023: KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kwa ushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania wamezindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Luninga ya flati Pamoja na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba
Airtel Money Timiza Akiba ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Money kuwweka akiba kidigital wakiwa popote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza kuzindua promosheni hiyo mpya, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema, ‘Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde inalenga kuhuisha na kuhamasisha wateja wa Airtel Money na jamii kwa ujumla kujijenga utamaduni wa kuweka akiba kidigitali. Airtel Money tunajisikia Fahari sana tunapoendeleza ubunifu katika huduma hii ya Airtel Money inayokuwa kwa kasi huku wateja wakijihudumia kidigitali kupitia Airtel Money, alisema Mmbando na kuongeza kuwa Airtel Tanzania imeshirikiana na Benki ya Letshego Tanzania kuendesha promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili (wiki 8) kuanzia leo.
Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde itawazadia wateja wote wa Airtel Money wanaoweka akiba kupitia Timiza akiba kuanzia wiki hii ambapo hadi kufikia mwisho wa promoshen wateja 203 watakuwa wameibuka washindi wa promosheni hii. Tutakuwa na droo moja kila wiki ambapo Wateja 25 watashijishindia sh 20,000 kila mmoja na tutawawekewa pesa zao za zawadi moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money, vilevile tutatoa zawadi ya bajaji mpya, pikipipiki mpya, pamoja na luninga mpya (flatscreen) kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii.
Mmbando aliongeza', “Mteja yeyote wa Airtel Money mwenye Timiza akiba ambaye anawekeza kuanzia shilingi 20,000 kwa wiki anastahili kuingia kwenye shindano na anaweza kushinda mara moja tu wakati wa droo ya wiki. Pia ninawakaribisha wateja wa Airtel Money ambao hawajawahi kutumia huduma ya Timiza Akiba kuanza kutumia sasa na kupata nafasi ya kujishindia zawadi hizi kabambe kila wiki.
“Wateja hawahitaji kujiandikisha au kulipa ili kuingia kwenye droo, utatakiwa tu kuweka akiba kwenye Airtel Money Timiza akiba kisha moja kwa moja utapata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia”. Alisema Mmbando
Nae Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Bi Leah Phil “Benki ya Letshego Tanzania tunajivunia ushrikiano wetu na Airtel Money kupitia huduma hii ya kujiwekezea kidigitali, tunawahakikishia wateja wote wa Airtel Money wenaotumia Timiza Akiba kwamba watapata zawadi zao za ushindi kwenye akaunti zao za Airtel Money zao mara tu watakapotangazwa kuwa washindi”.
Leah alieleza “Kuwekeza akiba ni rahisi Piga *150*60# chagua namba 6 kisha namba 1 na ubonyeze 3 uanze kuweka akiba kidigitali huku ukiwa umejiweka kwenye nafasi ya watakaoshinda Bajaji kwa mshindi wa Kwanza, Pikipiki kwa mshindi wa pili, Televisheni ya Kisasa kwa mshindi wa tatu au pesa taslimu za kila wiki
Leah aliongeza kuwa “Wateja watakaowekeza kupitia Timiza akiba pia watafaidika na riba ya hadi 4.5% kwa mwaka kwa kile kiwango watakachukwa wamejiwekea ndani ya Mwaka.Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Bi Leah Phil (wa pili kulia) wakionyesha bango baada ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kwa kushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania kuzindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Luninga ya flati Pamoja na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba. Kulia ni Meneja Masoko Benki ya Letshego Tanzania Uswege Mwaipyana na kushoto ni Meneja wa huduma wa Airtel Money Hellen Lymo.Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Bi Leah Phil (wa pili kulia) wakionyesha bango baada ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania kuzindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Luninga ya flati Pamoja na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba. Kulia ni Meneja Masoko Benki ya Letshego Tanzania Uswege Mwaipyana na kushoto ni Meneja wa huduma wa Airtel Money Hellen Lymo.Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Bi Leah Phil (wa pili kulia) wakionyesha bango baada ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania kuzindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Luninga ya flati Pamoja na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba. Promosheni hii inalenga kuhuisha na kuhamasisha wateja wa Airtel Money na jamii kwa ujumla kujijenga utamaduni wa kuweka akiba kidigitali.Meneja wa huduma wa Airtel Money,Hellen Lymo (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kwa kushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania kuzindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Luninga ya flati Pamoja na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba. Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) na (kulia) Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Bi Leah Phil .Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Bi Leah Phil (wa pili kulia) wakionyesha bango baada ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania kuzindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Luninga ya flati Pamoja na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba. Promosheni hii inalenga kuhuisha na kuhamasisha wateja wa Airtel Money na jamii kwa ujumla kujijenga utamaduni wa kuweka akiba kidigitali.
0 Comments