About Me

header ads

UJENZI NA UKARABATI WA VIVUKO KUTATUA CHANGAMOTO YA USAFIRI KANDA YA ZIWA

 

Imeelezwa kuwa kukamilika kwa ujenzi wa vivuko vipya vinne na ukarabati wa vivuko
vinne vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria kutapunguza
changamoto za usafiri kwa wananchi wanaoishi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na
kutarahisisha shughuli za maisha kwa urahisi, uhakika na usalama.

Hayo yamesemwa mkoani Mwanza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey
Kasekenya, wakati alipokagua karakana ya ujenzi wa meli na vivuko ya Songoro na
kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa vivuko hivyo vitavyogharimu
takribani bilioni 26 na kutarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.

“Nimekagua na nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vivuko vipya lakini pia na
ukarabati wa vivuko unaoendelea, nimatumaini yangu vivuko hivi vitakamilika ndani ya
muda kwani kuna baadhi ya maeneo vivuko hivyo havipo au kimebakia kimoja na hivyo
kutokidhi mahitaji ya wananchi", amesema Kasekenya.

Amefafanua kuwa kwa sasa ujenzi wa vivuko hivyo unaendelea na vipo katika hatua
mbalimbali na kutaja kuwa vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza),
Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na
Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Aidha, ukarabati wa vivuko unaoendelea ni pamoja na MV Misungwi (Kigongo - Busisi),
MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora -
Ukara).

Aidha, ameiagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kumsimamia mkandarasi
wa Kampuni ya Songoro kufunga vifaa vyote vilivyosanifiwa kuanzia katika hatua za
awali hadi vivuko hivyo vitapokamilika.

Naye, Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi kutoka TEMESA Eng. Aloyce
Ndunguru, amesema kuwa wanaendelea na ujenzi wa vituo vipya vitatu ambvyo ni
Bwiro (kisiwani) – Bukondo katika Wilaya ya Ukerewe, Kituo ch Ijinga (kisiwani) –
Kahangala katika Wilaya ya Magu na Kituo cha Mayenzi – Kanyinya ambapo miradi
hiyo ikikamilika itafanya wawe na jumla ya vituo 16 katika kanda hiyo.

Ameeleza pia kanda hiyo ina jumla ya vivuko 17 ambapo kati ya hivyo vivuko vinne vipo
katika matengenezo makubwa ambavyo ni MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara
(Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Songoro,
amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baadhi ya vivuko ambavyo vinafanyiwa ukarabati
vipo katika hatua za mwisho za kukalimika na vitarudishwa TEMESA mapema kwa ajili
ya kuendelea kutoa huduma.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi Eng. Aloyce Ndunguru, wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya vivuko vipya na matengenezo ya vivuko katika yard ya Songoro Marine, mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Songoro, akifafanua jambo kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, kuhusu ujenzi wa vivuko vipya vinne,
mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga –
Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo –
Kome (Buchosa - Mwanza).
Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi Eng. Aloyce Ndunguru, akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, kuhusu ujenzi wa vivuko
vipya vinne, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza),
Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na
Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, akikagua baadhi ya vipuli
vitavyofungwa katika vivuko vinne vinavyofanyiwa matengenezo/ukarabati katika yard
ya Songoro, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV
Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora -
Ukara).
Muonekano wa Kivuko cha MV Misungwi kinachotoa huduma katika eneo la Kigongo na
Busisi kikiwa katika matengezo katika yard ya Songoro, mkoani Mwanza.


Muonekano wa awali wa sehemu ya vivuko vinne vinavyojengwa na Kampuni ya
Songoro Marine, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe -
Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza)
na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Post a Comment

0 Comments