About Me

header ads

TRAMEPRO YATOA WITO WA USHIRIKIANO KATIKA WIKI YA HUDUMA 2026

Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO), Boniventura Mwalongo, amewataka wataalamu wa Tiba Asili nchini kuendelea kutoa huduma kwa uadilifu, weledi, huruma na kuzingatia usalama wa wananchi.

Akizungumza katika Wiki ya Huduma kwa wateja  2026, Mwalongo amesema huduma ni dhamana ya pamoja inayohitaji kujitolea, kusikiliza, kuheshimiana na kuwajibika, akisisitiza kuwa kila mgonjwa anayemtafuta mtaalamu wa Tiba Asili huja akiwa na imani na matumaini ambayo yanapaswa kulindwa.

Amesema wataalamu wanapaswa kuzingatia usafi, ubora wa dawa, maadili ya taaluma na usalama wa wagonjwa, huku wakiepuka ulaghai, ramli, ushirikina na ahadi zisizo na msingi wa kitaalamu.

Mwalongo amesisitiza pia uhusiano kati ya afya ya binadamu na afya ya mazingira, akiwataka wataalamu wa Tiba Asili kuwa mabalozi wa uhifadhi wa misitu, mimea tiba, maji na bioanuwai.

Aidha, ametoa wito kwa wanachama, wataalamu wa afya, watafiti, taasisi za elimu, vyombo vya habari na wadau wa mazingira kuimarisha ushirikiano katika utafiti, elimu, usalama wa dawa, Tiba Asili na uhifadhi wa mazingira.

“Tusijenge Shirika la viongozi pekee; tujenge Shirika la wanachama wote. Ushirikiano wetu ndio msingi wa kulifanya Shirika liwe na mchango mkubwa katika afya, mazingira na maendeleo ya jamii,” amesema.

Amesisitiza kuwa Wiki ya Huduma kwa wateja isiishie katika maadhimisho pekee, bali iwe mwanzo wa utamaduni wa kudumu wa kuhudumia, kusaidiana, kuheshimiana, kulinda afya na kutunza mazingira.

“Huduma ni wajibu wetu, upendo ni msingi wetu, afya na mazingira ni dhamana yetu.”

BONIVENTURA MWALONGO
Katibu Mkuu & Mtaalamu wa Tiba Asili – TRAMEPRO

Post a Comment

0 Comments