Wakulima wa mahindi nchini Tanzania wametakiwa kuhakikisha wanahakiki mbegu kabla ya kuzipanda ili kujikinga na mbegu bandia na zisizokidhi viwango, ambazo zinaweza kupunguza mavuno na kuwasababishia hasara kubwa.
Wito huo umetolewa jijini Mwanza wakati wakulima, wafanyabiashara wa mbegu na wadau wa kilimo walipokusanyika kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya kitaifa inayolenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kununua na kupanda mbegu za mahindi zilizothibitishwa.
Wakulima wamehimizwa kuhakikisha kuwa mbegu wanazonunua zimehakikiwa na kuthibitishwa na Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), ambayo ndiyo mamlaka ya kitaifa yenye jukumu la kusimamia ubora wa mbegu na kuhakikisha kuwa mbegu zinazouzwa kwa wakulima zinakidhi viwango vilivyowekwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayer Life Science Tanzania, Mwinyi Sango,amesema mabadiliko ya tabianchi yameongeza shinikizo kwa wakulima wadogo, hali inayofanya uchaguzi wa mbegu bora na zinazofaa mazingira husika kuwa muhimu zaidi katika kuongeza tija ya kilimo.



0 Comments