Na Mwandishi Wetu,Michuzi Tv
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mariam Ibrahim amemshuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa , Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kupendekeza jina lake na Kamati Kuu ya chama hicho kulipitisha na hatimaye kushinda kwa kura nyingi.
Ametoa shukrani hizo kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali wa Chama hicho wakati wa Semina ya Uongozi na Maendeleo kwa madiwani wote wanawake wa Mkoa wa Pwani.“Nitumie nafasi hii kwa dhati ya moyo wangu kumshukuru Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kunipendekeza mimi na Kamati Kuu kurudisha jina langu na kuja katika Mkoa wa Pwani na kupigiwa kura nyingi.
“Waheshimiwa madiwani hatujaonana toka Uchaguzi mkuu ulivyopita hivyo naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru nyote kwa kura zenu za kishindo.Nasema ahsanteni sana,amesema mbele ya madiwani hao pamoja na viongozi wa Mkoa huo.
Amesisitiza ameamua kutoa shukrani hizo kwasababu ndio mara yake ya kwanza wanakutana ambapo ametumia nafasi hiyo pia kuwaaahidi kuendelea kushirikiana nao na yupo tayari kwa wakati wowote ambao atahitahika.“Tutakuwa pamoja katika kila hali.”









0 Comments