WACHEZAJI wa timu ya Kikapu Dar City wamekutana na kupata chakula cha Pamoja na Mchezaji Mkongwe wa Klabu ya Manchester United, Rep Fernandez Jijini Dar es Salaam.
Katika hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano wa michezo kati ya Tanzania na Uingereza, gwiji wa soka Rio Ferdinand amekabidhiwa jezi maalumu ya timu ya kikapu ya Dar City na Mchezaji wa timu hiyo ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabeet.
Tukio hilo liliashiria mwanzo wa ushirikiano mpana wenye dhamira ya kuendeleza mchezo wa kikapu nchini, kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya michezo, pamoja na kuunganisha wadau na taasisi za michezo kutoka Tanzania na Uingereza kwa kiwango cha kimkakati chenye tija.
Katika mazungumzo yao, Thabeet na Ferdinand walijadili mikakati ya kisasa ya kukuza vipaji kupitia programu shirikishi, kuimarisha miundombinu ya mafunzo na matumizi ya teknolojia katika maendeleo ya wanamichezo.
Pia walisisitiza umuhimu wa kujenga mifumo endelevu ya mafunzo, kliniki za michezo, na programu za kubadilishana uzoefu wa kimataifa ili kuwapa vijana fursa pana zaidi


.jpeg)

0 Comments