About Me

header ads

FCC yaendelea Kuchochea Ukuaji wa Uchumi Kupitia Udhibiti wa Bidhaa Bandia

Na Mwandishi Wetu 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogoro amesema Tume ya Ushindani (FCC) kuongeza watumishi kutokana na majukumu yake kuwa makubwa ikiwemo kuongezeka kwa shehena katika  Bandari ya Dar es Salaam.

Mpogoro ameyasema hayo   wakati akiwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila  kufungua Semina ya Wahariri iliyoandaliwa na Tume ya Ushindani (FCC) jijini Dar es Salaam .

Amesema FCC chombo ambacho kinaangalia uchumi wa soko pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora.

Mpogoro amesema kuwa zamani kulikuwa na kuwepo kwa luninga zisizo na ubora lakini FCC imefanya kazi yake.

Aidha amesema kuwa FCC Wahariri  ni njia muhimu katika kuwa daraja la kufanikisha kutoa elimu kwa wananchi juu majukumu ya FCC.

Mpogoro amesema kuwa FCC Wilaya ya Ilala itaendelea kushirikiana na FCC  kwani Ilala ndio lango la bidhaa za nje na ndani katika kuendelea kuwepo kwa ushindani wa soko.
Nae Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa FCC Khadija Ngasongwa amesema  FCC inatoa Semina kwa Wahariri  ili kuwa njia ya kuhakikisha  wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusiana na FCC 

Amesema kuwa semina hiyo wahariri wapitishwa katika sheria ya ushindani 2003 ili wajue majukumu yake pamoja na sheria wanayotaka kupeleka bungeni ya Uhafueni.

Khadija amesema kuwa FCC inafanya kazi na taasisi zingine za kiudhibiti ikiwa ni kuhakikisha bidhaa zinaendelea kuwa bora na zenye ushindani wa soko .


Amesema  kuwa FCC haiko tayari kuona soko linapangwa na kufanya wananchi waweze kuumia katika upatikanaji bidhaa.

Amesema  Serikali  ya Awamu Sita imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji  hivyo ni wajibu FCC kuona maono ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  yanatekelezwa.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)Bakari Kimwanga amesema  kuwa semina  hiyo ni muhimu sana katika kuendelea kuilinda nchi yetu katika kuendelea kuwepo kwa soko la ushindani.

Bakari amesema kuwa FCC imefanya jambo la msingi katika kushirikisha wahariri katika kuendelea kutoa elimu ya ushindani wa soko nchini.



















 

Post a Comment

0 Comments