About Me

header ads

Mhandisi Jafari ajitosa kupambana na Babu Tale

 

Mhandisi na kada wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) Jafari Iddy Fadhili Hegga ( pichani kushoto) amechukua na kurudisha   fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo la  Morogoro Kusini Mashariki.

Awali, Mhandisi Jafari alikabidhiwa fomu  na katibu wa CCM wilaya comrade Michael Bundala na kufanikiwa kuirudisha.

Anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea wanaowania nafasi hiyo inayoshikiliwa kwa sasa na Mbunge aliyemaliza  muda  Hamis Taletale ( Babu Tale)

Mhandisi Jafari amesema  ameguswa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo na kuwaletea maendeleo kwa haraka kwa kushirikiana na viongozi wa chama jimboni humo pamoja na Serikali.

" Nikiwa kijana mwenye nguvu na kubobea katika mikakati ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi nimeona wakati umefika wa kuwa mtumishi wa watu wa jimbo hili,"

" Hivyo, naomba ridhaa ya chama changu na wananchi kunipokea kwa mikono miwili ili tujiletee maendeleo ya haraka,", amesema.

Post a Comment

0 Comments