Bandari ya Kemondo iliyopo Ziwa Victoria kwenye Tarafa ya Katerero wilayani Bukoba ni moja ya Bandari kubwa 10 Tanzania na ni Bandari yenye eneo kubwa sana. Kihistoria hii ni moja ya Bandari kubwa na kongwe Tanzania lakini bado ilikua duni ikipokea meli ndogondogo, boti na mitumbwi na ilikua haiwezi kupokea meli kubwakubwa.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amefanya ziara ya aina yake kwenye Tarafa ya Katerero kwa kutembelea kukagua ukarabati wa Bandari hii ya Kemondo uliogharimu takribani Bilioni 20 chini ya Mkandarasi Kampuni ya Kichina China Railway Major Bridge Engineering Limited.
RC Mwassa na viongozi aliombatana nao walipokelewa na Kaimu Mkuu wa Bandari Bw. David Nicodem na kutembezwa kukagua maeneo yote ya bandari.
Akipokea taarifa ya ukarabati wa Bandari hiyo, RC Mwassa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Bilioni 20 alizoleta Bandari ya Kemondo kuikarabati kwa kuongeza gati kubwa zenye uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi, ujenzi Jengo la Kisasa la abiria na Jengo la mizigo.
RC Mwassa aliambatana na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto aliyeambatana pia na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku, Mtendaji wa Kata ya Kemondo Ndugu Cyriacus Sosthenes na viongozi wengine.
0 Comments