About Me

header ads

STAMICO YAPONGEZWA KWA KUWEZESHA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA-PEMBA

 


Na Nasra Ismail

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Chamalangwa-Pemba Visiwani Zanzibar yaliyoanza tarehe 7/1/2025-15-1-2025 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Utalii na Malikale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mudrik Soraga.

Katika Maonesho hayo, Mgeni Rasmi alilitunuku Shirika la Madini la Taifa Cheti cha Ushiriki na Udhamini wa Maonesho hayo ikiwa ni is ishara ya kusamini mchango wa Shirika katika kuwezesha kufanyika kwa maonesho aidhaa STAMICO imeshiriki kwa ukubwa wake kupitia Mradi wa nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes.

Aidha, wageni mbalimbali waliofika katika Banda la STAMICO wameshuhudia uwekezaji Mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita kupitia Shirika la Madini la Taifa STAMICO katika kubuni,kuzalisha na Kusambaza Nishati Safi na Salama ya Rafiki Briquettes.


Post a Comment

0 Comments