About Me

header ads

Serikali Yakipongeza Chuo Cha Ufundi Arusha kwa Ubunifu wa Program zake.

Na Jane Edward, Arusha 

Serikali imesema inaunga mkono Dhamira ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)ya kuongeza program mpya na udahili hasa katika ngazi ya ufundi Sanifu huku akiitaka bodi ya shule hiyo kuendelea kuboresha mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la viwanda kwa sasa.

Hayo yameelezwa na Profesa Daniel Mushi ambaye ni katibu Mkuu wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa sherehe za mahafali ya 16 ya Chuo hicho.

Amesema kwa kuongezeka kwa program mpya ya udahili kunaongeza fursa kwa vijana kuweza kuendelea kujifunza fani ambazo wanazihitaji zinazoendana na kasi ya ulimwengu wa sasa.

Aidha amebainisha kuwa wahitimu hawana budi kuwa waadilifu,wazalendo,wachapakazi na kuheshimu dhamana watakayopewa ili kutoa huduma kwa jamii na kuwa waaminifu na kukiletea Chuo hicho Heshima.

"Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taifa kwa ujumla vinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) katika Ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya Serikali hapa nchini na kubwa zaidi ni kuzalisha wataalam katika ngazi ya Ufundi Stadi, Astashahada, stashahada na shahada"Alisema Prof Daniel



Post a Comment

0 Comments