About Me

header ads

BOT yatoa Mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki kwa taasisi za Kifedha Jijini Arusha.

 

Na Jane Edward,Arusha

Bank Kuu ya Tanzania (BOT)imefanya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya utatuzi wa malalamiko ya wateja kutokana na  huduma za fedha zinazotolewa kwa taasisi za kifedha zilizopo Jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa taasisi za fedha Aristedes Mrema Meneja idara ya uchumi Bank ya Tanzania Tawi la Arusha amesema Bank Kuu ya Tanzania ina jukumu la kusimamia taasisi za fedha pamoja na kuwalinda ambapo mfumo huo utazinduliwa Januari 2025.

Amesema kuwa Bank kuu ya Tanzania imeamua kufanya mchakato hio ilu kushughulikia malalamiko yanayotolewa na wateja na uweze kutumika kwa ufasaha hali itakayofanya shughuli za kifedha kufanyika kwa urahisi.

Amesema Mfumo wa kielektroniki utakuwa unatumiwa na taasisi za fedha pamoja na wateja wa taasisi za fedha ambapo kwa kutumia mfumo huo utawezesha kuboresha mchakato wa kushughulikia malalamiko ya watoa huduma za kifedha nchini.

"tumepokea malalamiko kwa mtu akitaka kuomba balance anacheleweshewa hapewi kwa wakati wanakuwa wanamzungusha,lakini pia kuchukuliwa fedha kwenye akaunti kwahyo mteja anakuwa haelewi kwahyo mteja anakuwa analalamika"Alisema Mrema

Aidha amesema faida za uwepo wa mfumo huo wa kielektroniki ni kurahisisha mteja kutoa malalamiko na kufatilia kwa kutumia mfumo huo hali ambayo itarahisisha matumizi ya muda.

"Mfumo huo ni mahsusi kwaajili ya taasisi zinazotoa mikopo na ni maalumu kwa wale wanaokopa kwenye taasisi hizo lengo ni kupunguza malalamiko"Alisema

Kwa upande wao watoa huduma za kifedha Imelda Mathew anasema mfumo huo utawasaidia kwakuwa wateja walikuwa wanatumia gharama kubwa kufatilia malalamiko yao kama yamefanyiwa kazi lakini uwepo wa mfumo huo utarahisisha matumizi ya muda.

Amesema changamoto zilizopo kwa sasa ni uelewa kwa wateja pamoja na  ucheleweshwaji wa marejesho hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya taasisi hizo za kifedha.




Post a Comment

0 Comments