Hayo ameyasema Msajili wa Bodi hiyo Mhandisi Bernard Kavishe wakati alipozungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuelekea wiki ya Wahandisi,jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Kavishe amesema kuwa katika mbio hizo wanatarajia kukusanya zaidi ya Sh.Bilioni Mbili ambazo zitakwenda kuchochea ufundishaji wa masomo ya Sayansi kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari.
Amesema kuwa ERB kuja na mpango ni kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya Wahadisi pamojà na kukua kwa Teknolojia katika sekta hiyo.
Amesema mbio hizo zitafanyika Septemba 7 mwaka huu katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Elimi,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda.
Mhandisi Kavishe amesema katika fedha hizo zitazopatikana wanatarajia kupeleka walimu Sayansi 100 wakujitolea katika Shule za Sekondari 26 nchini.
Amesema mpango huo walishaanza hivyo wanaongeza nguvu nyingine baada ya kufanya utafiti juu umuhimu wa walimu wa Sayansi ikiwa ni pamoja ya kuisaidia Serikali wakati inajipanga kuajiri walimu hao.
Aidha amesema kuwa mradi unaitwa SSP walianzisha wa Walimu hao wale wa shahada wa masomo ya Sayansi waliomba 152 ambapo uwezo wa ERB ulikuwa ni Walimu 20 wa kuweza kuwalipa posho.
Hata hivyo amesema kuwa walimu wa Sayansi ambao waliomba kwenda kujitolea wanalipa posho ya Sh.800,000 hadi 900,000 pamoja na kuwakatia Bima ya Afya.
Mhandisi Kavishe amesema Shule ambazo zilipata walimu hao ziliweza kutoa upendo kwa kuwapa Chakula na kuwakuza kitaaluma.
Amesema katika kwenda na usawa wa kijinsia kufikia 2030 kuwa na 50 50 wahandisi kuliko ilivyo sasa wakihamasisha wasichana kusoma masomo ya Sayansi.Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe akizungumza na Waandishi na Wahariri Vyombo vya Habari kuhusiana na Wiki ya Wahandisi itayoanza Septemba 1 hadi 7 ,jijini Dar es Salaam.
0 Comments