Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo amefungua kikao hiko na kueleza namna serikali ilivyotoa kipaumbele katika sekta ya kilimo na jinsi ilivyojipanga kuongeza uzalishaji wa mazao na bidhaa za kilimo.
"Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji, uchakataji na usafirishaji nje wa mazao ya kilimo na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa ugani."alisema
Katibu Tawala huyo amewaagiza wakuu wa Idara kuendelea kusimamia zoezi la upimaji wa udongo na kuhakikisha maafisa ugani wanatekeleza malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mtafiti wa Udongo kutoka TARI, Watson Matamwa, amesema hadi sasa afya ya udongo imepimwa Zaidi yay a mikoa 15 na kwamba udongo wa Mkoa wa Ruvuma umepungua rutuba na eneo kubwa la kilimo lina udongo wenye asidi nyingi, hali ambayo inasababisha kupungua kwa uzalishaji wa mazao.
Matamwa ameitaja Halmashauri ya Madaba wilayani Songea kuwa ina udongo wenye asidi kwa kiasi kikubwa, hali inayosababisha kuongezeka kwa matumizi ya mbolea na kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji yaliyowekwa na serikali.
Mtafiti huyo ameeleza tayari wameshatoa elimu kwa wakulima kutumia chokaa ili kukabiliana na hali hiyo na kulitaja zao la Soya kama moja ya mazao muhimu katika kuboresha afya ya udongo
Magnus Ndunguru mmoja wa wakulima walioshiriki kikao hicho, ameeleza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na ameiomba serikali kuendelea kuwawezesha wakulima kwa kuwasaidia kupata mitaji
Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kilimo cha kujadili zao la soya na upimaji wa afya ya udongo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Heritage Coltage mjini Songea ,kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Deo Sibula
Baadhi ya wadau wa kilimo kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kilimo
0 Comments