Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameyataja mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo katika ngazi ya Mkoa, Taifa na kimataifa
Hayo yamesemwa katika hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile katika Jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Ametaja mashirika hayo kuwa ni muhimu katika sekta ya maendeleo sio tu hapa nchini bali pia duniani kote ambapo ameyaasa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na miongozo ya serikali ili kufanya kazi bila ya kuvunja sheria
“Mnapotekeleza majukumu yenu zingatieni uwazi, Uwajibikaji, kuripoti kwa wasajili wasaidizi ngazi ya Mkoa na Halmashauri, na kupeleka taarifa ya mpango wa bajeti ya shirika Katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa’’,alisisitiza
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo ameyaomba mashirika yote yasiyo ya kiserikali kuhakikisha yanatambulika na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha ustawi na usalama wajamii na watanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Ruvuma Aidan Mbilinyi amesema wamejipanga kuhakikisha mashirika hayo yanafuata matakwa ya Serikali ili kuweza kuratibu kazi zao kwa kufuata sheria ,kanuni na taratibu zilizowekwa .
Mkoa wa Ruvuma una mashirika yasiyo ya kiserikali 182 ambayo yamesajiliwa kisheria na mashirika 7 ya nje yanayofanya kazi katika Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma yakijishughulisha na shughuli mbalimbali kama afya, elimu na kilimo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile akizunguza kwenye ufunguzi wa Jukwaa la mashirika yasiyokuwa yakiserikali Mkoa wa Ruvuma ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo akizungumza kwenye ufunguzi wa Jukwaa la mashirika yasiyokuwa yakiserikali Mkoa wa Ruvuma ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
baadhi ya wadau kutoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye kikao ukwaa la mashirika yasiyokuwa yakiserikali Mkoa wa Ruvuma ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
0 Comments