Berega, Kilosa
Rais Samia alisema anaipongeza TAMISEMI kwa kazi wanayoendelea kufanya ikiwemo uendelezaji wa miundombinu maeneo ya vijijini kupitia TARURA.
“Nimpongeze sana sana Mhandisi Seff, wataalam na timu yake ndani ya TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya Tanzania nzima, nimemvisha maua yake”.
Aidha, ameishukuru kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Limited na kampuni ya kizalendo ya SMARCON kwa kushirikiana na Pendharkar & Associates Limited kwa usimamizi wa mradi huo.
"Nawashukuru wakandarasi na wasimamizi wote kwa ujenzi wa daraja hili zuri”, amesema Rais Dkt. Samia.
Amesema kwamba daraja hilo litasaidia kuwaunganisha wananchi lakini kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Hata hivyo amewataka wananchi kutunza daraja hilo na amewaomba wasichimbe michango ili liweze kutumika miaka mingi kwa vizazi na vizazi.
Pia amewataka wananchi kutoharibu mazingira ya mto huo na wasichimbe mchanga chini ya daraja hilo kwani kwa kufanya hivyo watalipunguzia nguvu daraja hilo na pia kutanua mto.
“Wananchi mnaharibu mazingira, fanyeni shughuli zenu kwenye mto lakini msiharibu mazingira msichimbe mchanga kwenye mto huu, daraja hili limechukua fedha nyingi ili wananchi mnufaike, tunzeni daraja hili “, alisisitiza
Ameongeza kusema kwamba wananchi watakapochimba mchanga ndani ya mto watapunguzia nguvu daraja hilo.
0 Comments