Wajasilamali zaidi ya 100 wanaosimamiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) wamepatiwa mafunzo na Tume ya ushindani (FCC) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Afisa Mlinda Mlaji Mkuu (FCC) Bi. Magdalena Hall amesema kuwa wameweza kuwapatia mafunzo hayo ikiwa ni muendelezo wa kuwapatia elimu wafanyabiasha ili watambue na kuielewa FCC.
Bi. Magdalena Hall amesema kuwa mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wajasiliamali hao maana wao ni wazalishaji wa bidhaa na niwalaji wa mwisho.
Amesema kuwa ni wajibu wa wajasiliamali hasa wazalishaji kujua wajibu wao na kujisajili ili watambulike FCC maana ni wajibu kulinda nembo zao.
"Tunatoa wito kwa wajasiliamali hasa wazalishaji kuja Tume ya Ushindani wakisajili na watambulike ili bidhaa zao ziweze kulindwa kisheria na ziwaletee mafanikio", amesema Bi. Magdalena Hall.
Ameongeza kuwa ni vyema wajasiliamali kujua mikataba wanayoingia ni lazima isajiliwe na FCC ili kulindwa kisheria.
Kwa upande Bw. Christopher Dionis ambaya ni mmoja wa wajasilimali hao ameishukuru Tume ya Ushindani kwa elimu waliyoipata ambayo itachangia katika kuboresha bidhaa zao ili kukuza uchumi wa Nchi.
0 Comments