
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Dhamira ya Tanzania ni kukuza na kuendeleza amani na usalama barani Afrika ili kukuza na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi kwa jamii na bara zima la Afrika.
Hayo ameyasema leo Mei 25,2024 wakati wa akifungua maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika (PSC-AU).
"Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwenye vipaumbele vyetu tulivyojiwekea kama baraza ili kuendelea kutoa ushirikiano kwa nchi zilizojiunga katika baraza"
Maadhimisho yanatoa fursa kwa waafrika kutoa maoni yao ya kuimarisha baraza hilo linaloketi chini ya mwenyekiti wa baraza hilo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr.hmwinyi @ikuluzanzibar @maelezonews @africanunion_official @jmakamba @wizara_mambo_ya_nje_tz @wizara_ya_ulinzi_na_jkt.

.jpeg)

.jpeg)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofautitofauti wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) yaliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam leo Mei 25,2024.
.jpeg)





0 Comments