About Me

header ads

RPC LUTUMO AMEKEMEA VITENDO VINAVYOASHIRIA RUSHWA KWA ASKARI POLISI PWANI

 

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani






Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Pius Lutumo amekemea vitendo vyenye viashiria vya rushwa kwa askari polisi ,na kusisitiza hatowafumbia macho askari watakaobainika kujihusisha na kuomba ama kupokea rushwa.

Amewaasa askari polisi mkoani humo ,kuichukia rushwa na kuwataka wafanye kazi kwa kuheshimu sheria za nchi na maadili ya utumishi wa umma.

Lutumo alitoa rai hiyo, wakati akizungumza na maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya ukaguzi kwa wilaya za Mkoa wa Pwani.

Lutumo, alieleza jukumu la askari ni kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na kushindwa kufanya hivyo husababisha jamii kukosa imani na Jeshi la Polisi.

"Nasisitiza sitosita kuchukua hatua za kinidhamu kwa askari yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kuomba ama kupokea rushwa,

"Kila mmoja wenu akafanye kazi na kuwatumikia wananchi kwa haki na kulinda usalama pasipo rushwa,na sisitiza watumikieni wananchi pasipo kuomba rushwa kwani sitomvumilia atakaebainika kufanya vitendo hivyo" alielezea Lutumo.

Kadhalika, Askari hao wamekumbushwa kutimiza wajibu wao katika kuchukua hatua kwa mtu yeyote anae vunja sheria pasipokuwa na muhali, hususani kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto kupitia barabara kuu za Mkoa wa Pwani.


Post a Comment

0 Comments