Na Mwamvua Mwinyi,Pwani Machi 17
Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Kisiju ,Kata ya Kisiju ,Mkuranga mkoani Pwani ,bado kaa la moto ,kizungumkuti kwani umechukua muda mrefu huku wananchi wakiwa katika sintofahamu.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara ,Mkoani humo, wameonesha kutoridhishwa na muenendo wa mradi wa ujenzi huo ambao unatekelezwa na mamlaka ya bandari nchini TPA .
Hali hiyo imejidhirisha kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa jengo la Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani .
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir ,aliibua hoja kwa nini ujenzi wa bandari hiyo imekua ikisuasua huku Kila mwaka TPA (Mamlaka ya Bandari nchini )ikitenga fedha kwa ajili ya mradi huo.
'"Mradi huu unadaiwa kusuasua licha ya kutengewa fedha za ujenzi wake na Mamlaka ya Bandari nchini TPA kila mwaka."
Alieleza, mwaka wa fedha ulioisha ilitengwa sh. Bilion. 1. 2 (Moja nukta mbili) na mwaka huu wa fedha zimetengwa sh. Milioni 500.
Hoja hiyo ni moja ya hoja iliyohitaji pia kutaka kujua msimamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) .
Mwenyekiti wa CCM ,Mkoa wa Pwani Mwishehe Mlao akitoa tamko la chama kwa changamoto hiyo alisema CCM haiungi mkono wananchi kunyanyasika kwa kucheleweshewa huduma za bandari ili hali shughuli za kiuchumi zinakwama na kurudisha nyuma maendeleo ya watu.
Mkuu wa Mkoa Pwani - Abubakari Kunenge aliitaka TPA kupanga siku ,mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wafike Kisiju na kuwaeleza wananchi ukweli na sio kuahidiwa na TPA kila mara kuwa wanakamilisha ujenzi ndani ya muda mfupi wakati uhalisia ukiionekana wazi ujenzi bado utachukua muda.
0 Comments