Na Ismaili Luhamba
Jamii imeaswa kutoa sadaka kwa moyo hata kama kidogo ili kila mmoja aweze kuishi katika mazingira mazuri hususani wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.
Hayo ameyasema jana Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2024 Ahmed Misanga wakati taasisi yake ilipotoa sadaka katika kituo cha malezi cha Masjid Farouq Magorofani Wilayani Manyoni mkoani Singida. Misanga amesema kuwa kutoa ni moyo hakuhitaji uwe na mali nyingi, na namna ya kuoneana huruma endapo mwenzako unamuona hana kitu basi unaweza kumsaidia.
" Tunatoa sadaka kwa jamii pia naomba jamii ifahamu kuwa kusaidia watu hakuhitaji uwe na mali nyingi bali moyo wako tu uwe unahitaji kusaidia pale unapomuona mwenzako hayupo katika wakati mzuri, leo hii Ramadhani Charity Program tupo hapa manyoni ili kusaida watu wenye uhitaji maalumu, " Misanga
Katika hatua nyingne Misanga amewaomba jamii kuacha kuingia katika maadili mabaya kwani kuwa kwa sasa kumekuwa na mmomonyoko wa maadili amesema Qruan ndio inaweza kuwakomboa jamii ikawe watu bora.
Katika hatua nyingine ameisisitiza jamii kutafuta elimu popote walipo wa kiume na wakike kwa jitihada zozote kwani hata katika vitabu vya dini vimeelezea kuitafuta elimu ya dunia na akhera.
Katika hatua nyingine Mlezi wa Kituo hicho ambacho kimepewa msaada huo Mjumbe wa mkutano mkuu Jumuiya ya wazazi wa Taifa pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Jamal Juma , ameishukuru Ramadhani charity Program lakini pia wametumia fursa hiyo kumuombea Rais Dokta Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake chote atakachokuwa madarakani.
Malengo makubwa ya kituo hicho kujenga Chuo cha Ufundi Stadi maarufu kama VETA ili jamii ipate elimu itakayowasaidia kujiendeleza katika maisha yao.
Kwa upande wake Omary Kinyeto amewapongeza watoto hao kwa subra walioinyesha na kusisitiza kuendelea na nidhamu kwani nidhamu ndio silaha ya kila mtu katika kuishi vyema na jamii.
Mwalimu anayefundisha katika kituo cha cha malezi cha Masjid Farouq Magorofani Wilayani Manyoni Sheikh Salim Itara amesema katika kituo chake kuna watoto mbalimbali yatima na wasio yatima ambao wamekuja kutafuta elimu kwa msaada walioupata utasaidia kusogeza mbele gurudumu la maisha ya watoto hao. Kwa msaada huu mliotupatia utasaidia watoto wetu katika chakula ninayo furaha sana kwa msaada huu, " Sheikh Salim Itara
Taasisi ya Ramadhani Charity Program 2024 imetoa msaada wa mchele, Sukari, tende, unga, Luku kwa ajili ya umeme pamoja na pesa za mboga. Taasisi hii inafanya harakati za kutoa misaada hii kila mwaka na mwaka huu tayari imetoa misaada kwa mikoa mitano na inaendelea kutoa hadi mwisho wa mwezi mtukufu.
0 Comments