Wanafunzi wa shule ya sekondari Uhamiaji iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam wakiwa katika somo la utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Polisi, Kitengo cha Dawati la Jinsia kata ya Kawe, ASP Elizabeth Msabira, akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu vizuri wakati wa mafunzo ya elimu ya kupinga vitendo vya ukatili katika shule ya msingi Tumaini.
Wakufunzi wa mafunzo hayo wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wilayani Temeke katika shule ya msingi Mgulani.
Wanafunzi wa shule ya Mgulani wakisikiliza elimu ya utambuzi wa ukatili wa kijinsia inayotolewa na Maofisa kutoka madawati ya jinsia ya Jeshi la Polisi.Wanafunzi kutoka baadhi ya shule za sekondari na msingi katika mkoa wa Dar es Salaam wanaendelea kunufaika kwa kupatiwa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia na utambuzi wa vitendo hiyo, inayotolewa na Jeshi la Polisi, kwa udhamini wa kampuni ya Barrick, ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayoendelea.
Shule ambazo Maofisa kutoka madawati ya kijinsia ya Jeshi la Polisi tayari wamefikisha elimu hiyo ni shule ya msingi Tumaini Kawe, Mbezi Beach, Mgulani na Sekondari za Daniel Chongolo na Uhamiaji. Mafunzo haya yataendelea kufikia shule mbalimbali za msingi na sekondari na kwenye jamii zenye mikusanyiko ya watu wengi kwenye kipindi hiki cha maadhimisho hayo.
0 Comments