Na Mwandishi Wetu, Hanang.
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo 1000, mabati 800 na saruji mifuko 600 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Kateshi wilayani Hanang mkoani Manyara.
Vifaa hivyo vya ujenzi vyenye jumla ya thamani ya Sh.milioni 70 vimekabidhiwa leo Desemba 28,2023 wa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja ameishukuru Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kutoa vifaa vya ujenzi ambavyo kwa sasa ndivyo vinahitahika zaidi.
“Kwa niaba ya Serikali anachukua nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa Puma Energy Tanzania kwa kufika Kateshi kutoa misaada wa vifaa vya ujenzi.Tumepokea mifuko ya saruji 600, bati pisi 800 na nondo 1000.
“Vifaa hivi vya ujenzi vitasaidia eneo la ujenzi kwani tunakusudia kuanza ujenzi hivi karibuni kujenga nyumba za waathirika wale ambao wamepoteza makazi na mchango huu una thamani ya Sh.milioni 75,”amesema Mayanja.
Ameongeza kuwa msaada huo wa nondo, bati na saruji unakwenda kuongeza nguvu katika jitihada za Serikali za Awamu ya Sita chini ya ya Dk.Samia Suluhu Hassan ambayo imeamua kujenga nyumba kwa waathirika baada ya kutokea mafuriko Desemba 3, 2023
Aidha amesema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani wamekuwa wakipokeza zaidi msaada wa mahitaji ya chakula na dawa lakini kwa sasa wako kwenye hatua za mwisho kuanza ujenzi wa nyumba za waathirika kwa kutambua baada ya mafuriko kuna baadhi ya makazi yameharibiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Bi Fatma Mohemed Abdallah, Meneja Uhusiano wa Puma Energy Tanzania Limited Godluck Shirima amesema bodi ya wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake Dk.Selemani Majige, Menejimenti ya Kampuni chini ya uongozi wa Bi Fatma Mohamed Abdallah, wafanyakazi na wadau wote wameguswa na kuhuzunishwa na mafuriko yalio wakuta wananchi wa Katesh.
“Hivyo viongozi wetu wakatuelekeza kuleta msaada huu wa vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi na jitihada za Serikali kuwajengea makazi waathirika waliopoteza makazi yao kwenye mafuriko.
“Puma Energy pia ni muathirika wa mafuriko haya, ambapo kituo chao cha Kateshi kiliharibiwa na mafuriko, kwa hiyo kama waathirika na mkazi wa Kateshi, kampuni iliona ni vyema kutoa mchango wake kwa jamii ya Katesh,”amesema Shirima.Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja (wa tatu kushoto) akipokea bati kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambaye ni Meneja Uhusiano Godluck Shirima( wa pili kulia).Wanaoshuhudia Meneja Masoko Lilian Kanora(wa pili kushoto) na Meneja Rasilimali Watu Bw. Joseph Jaruma ( wa kwanza kulia).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Methew Giramisi .Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja (wa pili kulia )akipokea mfuko wa saruji ukiwa ni sehemu ya mifuko 600 ya saruji kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambaye ni Meneja Uhusiano Godluck Shirima( wa tatu kushoto) Meneja Masoko Lilian Kanora(wa kwanza kulia) na Meneja Rasilimali Watu Bw. Joseph Jaruma ( wa pili kushoto).Wa kwanza kulia ni Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Methew Giramisi.
0 Comments