About Me

header ads

DCPC yatoa furaha kwa watoto wanaoishi mazingira magumu

Na Mwandishi Wetu

Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kimetoa msaada kwa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Umra kilichopo Mwembechai jijini Dar es Salaam.

Msaada huo ni vyakula ,Sabuni ,Sukari ,nnguo pamoja na viatu ambavyo vitu hivyo vimetolewa na waandishi wa habari wa chama hicho.

Akizungumza Mara baada ya kukabidhi kwa Niaba ya Kamati ya Utendaji na Wanachama wa DCPC jijini Dar es Salaam  Katibu Mkuu  Fatuma Jalala amesema kuwa waandishi ni sehemu ya jamii hivyo wanawajibika kwa jamii kwa kuangalia makundi yenye uhitaji ikiwemo kutuo cha Umra

Amesema msaada huo ni mwanzo wa kuendelea kutoa msaada katika makundi mengine kwa wanachama kuendeleza kufanikisha utoaji wa msaada huo.

Aidha amesema wanachama ndio nguzo inayoshikilia kufanikisha majukumu mbalimbali na kuwataka wasichiko kutoa misaada pale panapohitajika.

Fatuma amesema kuwa waandishi wamekuwa sehemu ya kuandika wengine wanaotoa msaada lakini sasa ni tofauti wa sisi wenyewe kusaidia jamii.

Mkurugenzi wa Kituo cha Umra Rahma Kishimba ameshukuru DCPC na kuwaomba waendelee kuwangalia kwa mara nyingine kutokana na mahitaji ya kituo hicho.

Amesema licha ya DCPC kujitoa ameomba Taasisi zingine kuiga mfano wa DCPC katika kusaidia makundi yenye uhitaji.

"Nimefarijika sana waandishi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika Umra hiyo ni mipango ya Mungu"amesema Kishimba"

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) Fatuma Jalala  (wa tatu kutoka kushoto akikabidhi Msaada kwa  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto wanaoshi katika mazingira magumu Umra Rahma Kishimba (katikati) ni Naibu Katibu Mkuu, Chalila Kibuda. Hafla ya utoaji wa msaada huo umefanyika, jumapili Desemba 3, 2023, kwenye kituo hicho, Magomeni, Mwembechai.


Baadhi ya matukio ya utoaji msaada kwenye kituo cha Umra

Post a Comment

0 Comments