About Me

header ads

PROF. NDALICHAKO AITAKA CMA KUZINGATIA SHERIA KATIKA UTATUZI MIGOGORO

 

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA na Idara ya Kazi kutatua migogoro ya wafanyakazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na miongozo ya serikali.

 Amesema changamoto za wafanyakazi na waajiri zimekuwa zikiwasilishwa ofisini kwakwe baadala ya kufanyiwa kazi na CMA kwa kushirikiana na Idara ya Kazi ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

 Prof. Ndalichako amebainisha hayo leo Novemba 11, 2023 katika ukumbi wa PSSSF Mkoani Dodoma wakati wa kikao cha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Watumishi wake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo.

Aidha, amezipongeza Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa  kufanya kazi kwa weledi, bidii na ufanisi katika  kufanikisha shughuri za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nina timu nzuri na wakati wowote ninapoitaka itekeleze jambo basi linatekelezwa kwa wakati na haraka sana” Amesema.



Baadhi ya Menejimenti ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) wakisikiliza kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha Waziri Mkuu na Watumishi wake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo leo Novemba 11, 2023 Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla akibadirishana Mawazo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma wakati wa kikao cha Waziri Mkuu na Watumishi wake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo leo Novemba 11, 2023 Mkoani Dodoma.

Post a Comment

0 Comments