About Me

header ads

TAKUKURU YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WAFANYABIASHARA SITA KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI WA FEDHA BILIONI 1.4

 


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imewafikisha mahakamani wafanyabiashara sita akiwemo raia wa Nepal
Bhusal Govinda, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi, likiwemo shtaka la utakatishaji wa zaidi ya Sh.bilioni 1.4.

Mbali na Govinda washitakiwa wengine Emanuel Gaudios, raia wa Cameroon Takoounga Anselme , Raymond Richard Caroline Magafu na Grace Sureshi.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo na Wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU Thuwaiba Hussein akisaidiana na Groria Mwenda wamedai washitakiwa walitenda makosa hayo kati ya Agosti na Septemba mwaka 2022, jijini Dar es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio, imedaiwa kuwa, katika tarehe hizo washtakiwa kwa nia ovu, walijiunga mtandao wa kiharifu na kujipatia USD 623,000 sawa na Sh.1,449, 098,000 kutoka kampuni ya Zhejiang Afol Import and Export Co. ltd.

Inadaiwa kati ya Agosti 19 na Septemba 29 mwaka jana jijini Caroline na Govinda walijipatia sh bilioni 1,449, 098,000 kutoka kampuni hiyo kupitia akaunti yao iliyopo benki ya Stanbick kama malipo ya kuuza madini aina ya shaba tani 100, kupitia kampuni ya Steca Export and Import wakati wakijua si kweli.

Aidha inadaiwa, washtakiwa Gaudios , Richard na Grace walikula njama ya kutenda kosa la kugushi na kugushi hati ya kusafirishia mzigo (bill of lading), akionesha kwamba, kampuni ya Stecas Export and Import, imesafirisha tani 44 za madini ya shaba kwenda kampuni ya Zhejiang Afol Import and Export Co.Ltd wakati akijuasi kweli.

Pia wanadaiwa kughushi hati ya kusafirishia mzigo, ikionesha kampuni ya Stecas Export and Import, imesafirisha tani 66 za madini ya shaba kwenda kampuni ya Zhejiang Afol Import and Export Co.Ltd wakati akijuasi kweli.

Mshtakiwa Gaudious akiwa mwajiriwa wa kampuni ya Glob Vest Group Ltd, alijipatia sh 12, 964,000 kutoka kampuni ya Zhejiang Afol Import and Export Co LTD kama malipo ya kusafirisha mzigo tani 44 za madini ya shaba.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha miamala ya sh bilioni 1,449, 098,000 wakati wakijua fedha hizo ni mazalia ya makosa ya jinai.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Mei 25 mwaka huu

Post a Comment

0 Comments