Na.Khadija Seif,Michuzi blog
PRESHA ya Kushuka na kupanda yawaingia warembo 16 kuelekea Fainali ya Miss Darzone 2023 mara baada ya kufichuliwa kwa zawadi ya gari aina ya Toyota Allion huku wakiomba pakuche ifike mei 13,2023 kushuhudia uhondo huo pale Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Michuzi Leo Mei 12,2023 Muwakilishi kutoka Kampuni ya Dalum Motors Baraka Mase amesema wanaunga Mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha ajira zinazalishwa kwa wingi pamoja na vipaji vinapewa nafasi ya kuonekana kwenye jamii.
Pia ameeleza shahuku yao kubwa ni kuona Mrembo atakaefanikiwa kushinda siku ya kesho Mei 13,2023 anakabidhiwa gari yake haraka na ndio sababu ya zawadi hiyo kufichuliwa eneo la ofisi za mdhamini huyo ili ikitokea ubabaishaji Mrembo aweze kufika ofisi hapo na kufanya madai.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa gari hiyo aina ya Toyota Allion ina thamani ya Shilingi Milioni 18 za kitanzania.
"Tutakwenda kumpatia Mrembo gari ya aina ya Toyota Allion yenye thamani shilingi milioni 18 pamoja na mrembo huyo kuwa balozi wa Kampuni yetu kwa muda wa mwaka mzima. ''
Aidha Mratibu wa Shindano hilo kutoka Kampuni ya We planners Linda Samson ameongeza kuwa wadau wote wajitokeze katika kumalizika kwa safari ya kupatikana Mrembo ambae atakidhi vigezo vyote kuanzia urembo pamoja na uwezo wa akili yake na kujitoa kwenye kazi za jamii.
"Tumebakiza masaa machache kufikia fainali ya Miss Darzone kwa warembo 16 ambao wamekaa kambini kwa siku kadhaa na kujifunza vingi ikiwemo nidhamu, jinsi ya kuitumikia jamii pamoja na mavazi anayoweza kuvaa Mrembo.
Pia amesema Kesho kutaambatana burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii pamoja na warembo wenye kupamba usiku huo .
0 Comments