|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa (kulia) akikabidhiwa moja ya chapisho la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) alipotembelea Banda la mtandao huo kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa (kulia), pamoja na mwenyeji wake, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (wa pili kulia) wakiwa kwenye Banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.
|
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa (kulia) akiipongeza sekretarieti ya TEN/MET alipotembelea banda lao kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Wanafunzi wakijisomea kwenye moja ya mabada yanayoshiriki maadhimisho hayo. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea Banda la Haki Elimu kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea Banda la Room to Read kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea Banda la Room to Read kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akizungumza na wanafunzi katika Banda la Hedhi Salama. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akizungumza na wanafunzi katika Banda la Hedhi Salama. |
|
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga Mwenyekiti wa Kamati ya GAWE 2023 Kitaifa, Greyson Mgoi pamoja na Mkuu wa Miradi, TEN/MET Martha Makala wakitembelea darasa la awali lililoandaliwa kwa mfumo wa kisasas na rafiki kwa kufundishia watoto. |
|
Wanafunzi wakiingia kwa maandamano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mvuha kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Wanafunzi wakiingia kwa maandamano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mvuha kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akihutubia wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Rebeca Nsemwa akihutubia wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro. |
Na Joachim Mushi, Morogoro
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuboresha utoaji wa elimu bora na jumuishi kwa kutumia rasilimali zake, Ruzuku kwa ajili ya maendeleo ya wanafunzi huku pia katika gazi ya wilaya ikitumia mapato yake ya ndani kwa maendeleo ya elimu wilayani ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa, vyoo vya wanafunzi na ujenzi wa nyumba za walimu.
Kaulihiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Rebeca Nsemwa alipokuwa akizinduwa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.
Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wazazi na jamii kuendelea kuchangia maendeleo ya shule hasa katika kujenga madarasa na nyumba za walimu hadi kufikia lenta ili serikali iweze kumalizia kujenga na kuweka vifaa vinavyohitajika kama madawati na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
"Pia tunatoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanagharamia chakula cha watoto wao shuleni. Hivyo kamati za shule zihakikishe zinasimamia na kuhamasisha wazazi/wananchi kuchangia chakula na kuhakikisha kinapatikana shuleni. Sambamba na hayo wazazi wanaaswa kuwezesha watoto wao kuhudhuria masomo bila kuwakatisha kwa kuwapa kazi saa za shule, kuwapeleka unyago au kuwaozesha. Sheria inakataza kuwaozesha wanafunzi na adhabu kali itatolewa kwa atakayekiuka." alisisitiza kiongozi huyo.
Aidha alitoa wito kwa Walimu na Wathibiti Ubora kufanya kazi zao kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu katika wilaya yetu na mkoa kwa ujumla, huku akibainisha kuwa Serikali ngazi ya Mkoa na wilaya iko tayari kutoa msaada wowote pale ambapo utahitajika.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga ambao ni waratibu wa juma hilo la elimu linatarajia kuongeza uelewa kwa umma juu ya umuhimu wa kuchangia ubo reshaji wa elimu, kuhamasisha serikali kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama watoto wenye ulemavu, watoto wa kike, kuboresha miundombinu ya kufundishia pamoja na kujifunzia.
Pamoja juma la elimu litahamasisha na kukumbusha jamii, serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau mbalimbali wa elimu kuhusu umuhimu wa uchangiaji wa elimu kwa kuzingatia kauli mbiu isemayo “Tuboreshe uwekezaji wa rasilimali za ndani kwenye elimu kwa maendeleo Endelevu.
0 Comments