Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mtaalam wa kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s Bw. Aurelien Mali, Jijini Dodoma. Katikati ni Kiongozi wa Timu hiyo Bw. John Walsh. Moody’s wapo nchini kuifanyia Tanzania Credit Rating.Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia), akisalimiana na Kiongozi wa jopo la wataalam waliowasili nchini kufanya tathimini ya uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, Bw. John Walsh, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizindua zoezi la Taasisi ya kufanya tathimiji ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, Jijini Dodoma. Kulia ni Kiongozi wa Timu hiyo Bw. John Walsh. Moody’s wapo nchini kuifanyia Tanzania Credit Rating.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kufanya Tathimini ya Uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) Bw. John Walsh (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Bw. Aurelien Mali na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justin. Kulia ni Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila, Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, baada ya kukutana Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi ya tathimini hiyo.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Fedha na Mipango
0 Comments