About Me

header ads

NAIBU WAZIRI KATIBA NA SHERIA ATEMBELEA LAW SCHOOL

 

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul (kulia) akisalimiana na baadhi ya wajumbe
wa Menejimenti ya Law School alipowasili kwenye taasisi hiyo juzi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kupata uelewa wa majukumu yanayotekelezwa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul (kushoto) akimsikiliza Naibu Mkuu wa
Taasisi, Prof. Zakayo Lukumay (katikati) kuhusu mfumo wa ufundishaji unaotumika Law School
alipotembelea taasisi hiyo juzi jijini Dar es Salaam. Kulia ni mhadhiri aliyekuwa darasani
akiwafundisha wanafunzi ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini,
Griffin Mwakapeje.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul (kushoto) akiwasalimia baadhi ya
wanafunzi wa Law School aliowakuta darasani wakiendelea na masomo katika taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul (kulia) akitembelea mazingira ya Law
School ili kuona miundombinu mbalimbali ya taasisi hiyo. Kushoto ni mwenyeji wake Naibu Mkuu wa
Taasisi, Prof. Zakayo Lukumay.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul (aliyesimama katikati) akiwa kwenye picha
ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Law School.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul (kulia) akipata maelezo jinsi ya kupata
machapisho ya kielektroniki katika maktaba ya Law School (computer lab) kutoka kwa mwanafunzi
wa taasisi hiyo (aliyekaa). Wengine pichani ni watumishi wa Taasisi hiyo.

Post a Comment

0 Comments