Na Mwandishi wetu.
Dar es Salaam. Mmoja wa wachezaji gofu maarufu wa kike, Queen Siraki ameibuka mshindi wa kiti cha Urais wa Chama cha mchezo wa gofu cha wanawake nchini (TLGU) katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi jioni kwenye klabu ya Lugalo.
Katika uchaguzi huo uliowashirikisha jumla ya wapiga kura 26 kutoka klabu mbalimbali, Queen alishinda kwa vishindo baada ya kupata kura zote 26 na kuchukua nafasi ya Sophia Viggo ambaye hakugombea.
Siraki ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Exim alisema kuwa amefurahi kushinda nafasi hiyo na kazi kubwa waliyokuwa nayo ni kuendeleza mchezo kwa ngazi zote, kuanzia ya chini mpaka kwa wakubwa.
“Nimefurahi kushinda kiti hiki na kazi yetu kubwa kwa sasa ni kuutangaza mchezo kwa wadau na kuendeleza kufikia hatua ya juu kabisa ya maendeleo. Kamati mpya ya utendaji imeundwa na viongozi wenye uchu wa maendeleo na naamini kwa ushirikiano, tutafikia malengo yetu,” alisema Siraki.
Mbali ya Siraki kuchaguliwa katika nafasi ya Rais, Ayne Magombe alishinda nafasi ya Makamu Rais kwa kupata kura 25 kati ya 26 huku nafasi ya katibu mkuu ikichukuliwa na Yasmin Chali aliyepata kura 24 kati ya 26 huku Joyce Ndyetabura akishinda nafasi ya mweka Hazina kwa kupata kura 25 kati ya 126 na Hawa Wanyeche akichaguliwa kuwa katibu wa mashindano kwa kupata kura 24 kati ya 26.
Kwa upande wake, Yasmin Chali alisema kuwa wana malengo makubwa sana ya kuendeleza mchezo huo hapa nchini na kuitangaza nchi nje ya mipaka yake kupitia mchezo huo.
“Tuna wachezaji wengi sana wenye vipaji ambao wana malengo ya kufikia hatua ya juu kabisa. Kazi yetu ni kuweka mipango ya maendeleo na kuwafanya wachezaji kuwa na furaha na pia kushiriki katika mashindano mengi zaidi, nchini na nje ya nchi pia,” alisema Yasmin.Rais mpya wa chama cha gofu cha wanawake Tanzania (TLGU), Queen Siraki (kushoto) akila kiapo mbele ya mwanasheria Frank Komba mara baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye klabu ya Lugalo .
Rais wa zamani wa chama cha gofu cha wanawake (TLGU), Sophia Viggo (wa tatu kushoto) akikabidhi katiba ya chama hicho kwa Rais mpya, Queen Siraki (wa tatu kulia) mara baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye klabu ya Lugalo juzi. Wanaoshuhudia zoezi hil ni Yasmin Chali (wa pili kushoto) ambaye ni Katibu Mkuu, Joyce Ndyetabura (wa kwanza kushoto) ambaye ni mweka hazina, Ayne Magombe ambaye ni makamu rais (Wa kwanza kulia) na katibu wa mashindano mpya, Hawa wanyeche wa pili kulia.
Makamu wa Rais mpya wa chama cha gofu cha wanawake Tanzania (TLGU), Ayne Magombe (kushoto) akila kiapo mbele ya mwanasheria Frank Komba mara baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye klabu ya Lugalo .
Katibu Mkuu mpya wa chama cha gofu cha wanawake Tanzania (TLGU), Yasmin Chali (kushoto) akila kiapo mbele ya mwanasheria Frank Komba mara baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye klabu ya Lugalo .
Mweka Hazina mpya wa chama cha gofu cha wanawake Tanzania (TLGU), Joyce Ndyetabura (kushoto) akila kiapo mbele ya mwanasheria Frank Komba mara baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye klabu ya Lugalo.
Katibu wa mashindano wa chama cha gofu cha wanawake Tanzania (TLGU), Hawa Wanyeche (kushoto) akila kiapo mbele ya mwanasheria Frank Komba mara baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye klabu ya Lugalo.
0 Comments