Jamii imeshauriwa kufanya uchunguzi wa afya mapema ikiwemo Homa ya Ini ili kubaini endapo mtu ameathirika aweze kuanza tiba mapema na endapo hajaathirika aweze kupata chanjo ili kujikinga na maradhi hayo.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. John Rwegasha kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akifungua kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya Homa ya Ini inayofanyika Machi 15 na 16, 2023 bila malipo, zoezi linalo ratibiwa na madaktari wa Muhimbili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Dkt. Rwegasha amebainisha kuwa takwimu zinaonesha Afrika Mashariki katika kila watu 100 watu nane wanaishi na virusi vya homa ya ini ambavyo husabisha kushambuliwa kwa ini ambapo tumbo huvimba na kujaa maji.
“Ugonjwa huu maambukizi yake hayajioneshi moja kwa moja badala yake mtu hupata magonjwa nyemelezi ikiwemo kutapika damu au ini lake kusinyaa hivyo tumeweka kambi hii kwa lengo la kujenga uelewa kuhusu Homa ya Ini ikiwa ni kuelekea kwenye kongamano la saratani ya ini litakalofanyika Machi 17 na 18, 2023” ameongeza Dkt. Rwegasha
Kwa upande wake Daktari Bingwa Mbobezi Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini Dkt. Eva Uiso amesema ugonjwa wa Homa ya Ini huambukizwa na njia zake za maambukizi hazitofautiani na za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Dkt.Eva ameongeza kuwa ili kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa Saratani ya Ini wameamua kufanya kongamano hilo ili kujadili na kuja mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo nchini.
Wananchi waliojitokeza kupima afya zao wameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuweka kambi hiyo ya uchunguzi na matibabu ya homa ya ini kwani imekuwa fursa kwao kujua hali zao kiafya.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. John Rwegasha akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za uchunguzi na matibabu ya Homa ya Ini. Kushoto ni Dkt. Omari Mwanga.
Moja mwananchi akiendelea na vipimo wakati wa kambi ya uchunguzi na matibabu ya Homa ya Ini inayoendelea Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya wananchi wakisubiri huduma katika kambi ya uchunguzi na matibabu ya Homa ya Ini inayoendelea Muhimbili.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. John Rwegasha akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
0 Comments