Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea watoto
kwa kuzingatia maadili ya kitanzania pamoja na kuongeza umakini katika
maudhui yanayooneshwa katika televisheni.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na waumini wa
Kijiji cha kasumo mkoani Kigoma mara baada ya kushiriki Ibada ya
kawaida ya katikati ya wiki katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria
Malkia wa Amani iliopo Kijiji hapo.
Amesema ni wazi kwa sasa kumekuwepo na changamoto ya
mmomonyoko wa maadili ikiwemo ndoa za jinsia moja ambapo wazazi,
walezi na jamii kwa ujumla inapaswa kukemea vikali ili kuondokana na
taifa lisilofaa kwa vizazi vya sasa na baadaye.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewaasa wananchi wa Kasumo na
Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutoa ushirikiano wakati huu ambapo
serikali inafanya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo
ambayo ni nyenzo muhimu kwa biashara na urahisi wa kufikia huduma
za jamii kama vile hospitali na shule.
Aidha amewataka kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ikiwemo kuzingatia
bei halisi za ardhi katika maeneo yao ili kutowapoteza wawekezaji hao.
Makamu wa Rais amewasihi wananchi wa Kasumo kujitolea kwa hali na
mali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kijijini hapo
ikiwemo ya huduma za afya.
Ibada hiyo iliofanyika leo tarehe 23 Julai 2023 imehudhuriwa na mke wa
Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango na kuongozwa na Paroko
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki
Ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira
Maria Malkia wa Amani iliopo Kijiji cha Kasumo mkoani Kigoma leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia
ya Bikira Maria Malkia wa Amani iliopo Kijiji cha Kasumo mkoani Kigoma
leo tarehe 23 Machi 2023 baada ya kumaliza kushiriki Ibada ya kawaida
ya asubuhi Kijiji hapo.
0 Comments