About Me

header ads

MAKAMU KUENDELEZA ZIARA MKOA WA KUSINI -UNGUJA

IMEELEZWA Kwamba kuibuka migogoro mingi ya Ardhi Zanzibar,
kunachangiwa sana na kuwepo ongezeko la wimbi kubwa la watafutaji
maisha sambamba na kuongezeka idadi ya watu, biashara na watafutaji
maisha na kuifanya ardhi ya Zanzibar kuwa na thamani zaidi kuliko
ilivyokuwa hapo awali.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud
Othman, ameyasema hayo huko Pongwe Jimbo la Tunguu wilaya ya Kati
Unguja alipokuwa akifanya majumuisho ya muendelezo wa zaira yake
ya kutembelea wagonjwa na waliopatwa na misiba katika Mkoa wa
Kusini Unguja.

Amefahamisha kwamba kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya wwaka
2012 hivi sasa Zanzibar inaidadi ya watu wapatao zaidi ya milioni moja
na laki tisa wakati 2012 walikuwa wastani wa watu milioni moja na laki
tatu aongezko ambalo ni zaidi watu laki saba.

Aidha Mhe. Othman amesema kwamba pia tatizo hilo linachangiwa na
kuwepo utaratibu wa usimamizi usiokidhi mahitaji katika wakati huu
jambo ambalo linachangia kuifanya ardhi kuwa ni mali ya kuwasaidia
watu wachache.

Mhe. Makamiu amesema kwamba kutokana na serikali kubaini kuwepo
hali hiyo na kuongezeka kwa matatizo mengi ya ardhi hivi sasa imeunda
kamati ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi ili kusaidia kupatikana haki
kwa muda mfupi kabla ya suala la namna hiyo kupelekwa mahakamani.

Aidha Mhe. Othman amewaonya wale wote wenye uwezo wasitumie
mahakama kuwadhulum wananchi ardhi zao kwa kuwa kufanya hivyo ni
jambo ovu lililokatazwa hata katika vitabu vitakatifu vya Dini.

Aidha Mhe. Makamu amewaomba wananchi kuendelea na utamaduni
wa kusaidiana hasa kwa wale wenye uwezo katika kipindi hiki cha
mwezi wa ramadhani ili kusaidia umoja na mshikamano miongoni mwa
wananchi mbali mbali.

Mhe. Makamu amewaomba wananchi kuiga mifano ya mkoa wa mjini
mkuanzisha mfumo wa faraja ambao utasaidia kutatua changamoto
mbali mbali hasa katika wakati wa shida zinapojitokeza ikiwemo hata
kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Awali Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Mkoa wa Kati Kichama Vua
Abdulkadir, akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa huo,
alimueleza Mhe. Makamu kwamba mkoa kusini hivi sasa kuna wimbi
kubwa la watu kunyanganywa ardhi zao na kwamba licha ya kesi nyingi
za aina hiyo kupelekwa mahakamani, lakini haki huwa haipatikani.

Amefahamisha kwamba kuwepo kwa hali hiyo kunachangia wananchi
wengi hasa wanyonge kutofaidika na rasilimali yao hiyo na kuendelea
kutumiwa na baadhi ya watu kwa njia ya kuwapora na wao kunufaika
zaidi.

Aidha amefahamisha kuwa suala hilo pia inachangia hali ya maisha ya
wananchi kuendelea kudorora na kuongezeka umasikini jambo ambalo
linahitaji viongozi waingilie kati kupatikana ufumbuzi wa masuala ya
namna hiyo.

Mhe. Othman katika ziara hiyo aliyombatana na baadhi ya viongozi wa
ACT-Wazalendo Akiwemo Kaimu Naibu Katibu Mkuu Salim Biman na
leo ametembelea majimbo ya Mkoa wa Kusini Unguja ambapo ni
muendelezo wa Utamaduni uliorithiwa kutoka kwa Mtangulizi wake
marehemu Maalim Seif Sharif Hamad ambao alikuwa akiufanya kila
ifikapo kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud
Othman akimsalimia mzee Kitisho Mahmoud Abdalla,wa Kumbini
Makunduchi wakati Mhe. Othman alipofika nyumbani kwa mzee huyo
huko Makunduchi kumjulia hali. Mhe. Makamu alikuwa katika ziara
Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 28.03.03 kuwatembelea wagonjwa
na waliofikwa na changamoto mbali ikiwemo misiba. Picha na Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais.

Post a Comment

0 Comments