Na Mwandishi Wetu,Same
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa elimu kwa lengo la kujadili changamoto zinazosababisha baadhi ya shule kuwa na matokeo yasiyoridhisha na kuja na mipango ya pamoja kukabiliana na changamoto hizo.
Akizungumza mbele ya kikao hicho maalum Mkuu wa Wilaya Kasilda Mgeni amewataka
kila mdau kutimiza wajibu wake, hasa wajibu wa wazazi kuchangia chakula shuleni, kufuatilia maendeleo ya Watoto wao na kudhibiti Utolo, walimu kutimiza wajibu wao kufundisha vipindi vyote Darasani lengo ni kuwasaidia wanafunzi wawe na uwelewa mpana kujibu mithihan yao kwa ufasaha.
Pia ameagiza viongozi wa Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi na kuwasimamia walimu kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Aidha ameonesha dhamira yake Kwa wadau wa elimu ya kuandaa tuzo na zawadi mbalimbali kama Motisha kwa Walimu na Shule zitakazo onekana kubadilika na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa,tuzo hizo zitatolewa Julai 30 mwaka huu ambapo mgeni rasmi atakua Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu.
0 Comments